Ijumaa, 9 Novemba 2018
HERI WALIO MASIKINI WA ROHO
HERI WALIO MASKINI WA ROHO
NENO LA MSINGI:
MATHAYO 5:3:
“HERI WALIO MASKINI WA ROHO; maana ufalme wa mbinguni ni wao”
<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><
S
ifa ya kidunia, ya kutuwezesha kuingia mahali pa heshima kubwa na pazuri, kwa mfano hoteli kubwa ya kitalii, ni kuwa tajiri. Tajiri, ana nafasi ya kufika karibu kila mahali duniani. Jambo hili, liko kinyume kabisa katika ulimwengu wa roho. Sifa ya kuingia mbinguni mahali penye heshima na uzuri usio kifani, ni kuwa MASKINI WA ROHO. Tunapokuwa MATAJIRI WA ROHO, basi tujue waziwazi kwamba, hatuwezi kamwe kuingia mbinguni au kuurithi ufalme wa mbinguni. Ni kwa sababu hii, leo katika ibada ya Kanisa la Nyumbani, tunachukua muda kujifunza nini maana ya umaskini wa roho. Tukifahamu maana ya umaskini wa roho, tutakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuhakikisha tunakuwa na sifa hii muhimu ya kutufanya tuingie mbinguni. Tunaweza kuufahamu umaskini wa roho, kwa kutafakari jinsi anavyokuwa mtu maskini katika hali ya kawaida:
MASKINI, NI MTU ASIYE NA KITU: Tukitaka kuingia mbinguni, hatuna budi kuja mbele za Mungu kama maskini tusio na kitu, tuliojaa mahitaji. Hatuna budi kuja mbele za Mungu, tukiwa hatujui chochote. Tukijiona tunajua, basi tunakuwa tunajifanya matajiri. Hatuna budi kuja mbele za Mungu kama watu tusiojua neno lolote la Mungu [1 WAKORINTHO 8:2]. Lakini, wako watu wengine ambao wakihubiriwa Neno la Mungu, upesi sana watasema kwamba wanajua kila kitu katika Biblia, na hivyo hawataki kusikia neno lolote. Tukiwa kama watu hawa, hatuwezi kamwe kuurithi ufalme wa mbinguni. Hatuna budi kuwa na utajiri wa kusikia Neno la Mungu, wakati wote; tukiwa wajinga kama wanyama [ZABURI 73:22,24] Siyo hilo tu. Hatuna budi pia, kuja mbele za Mungu huku tukikiri moyoni kwamba, sisi ni wenye dhambi; na kutubu dhambi hizo kwa kumaanisha moyoni, kuziacha kabisa. Tukija mbele za Mungu kama watu wasio na dhambi, tunajionyesha kwamba sisi ni matajiri na hatuna haja ya kitu, kumbe mbele za Mungu ni wanyonge mno [UFUNUO 3:17, 19]. Tukisema hatuna hatia, tunajidanganya wenyewe na kuingia hukumuni, maana sisi sote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu [YEREMIA 2:35;
1 YOHANA 1:8-10; WARUMI 3:23]. Tunapokuwa tayari kuziungama dhambi zetu, ndipo tunapopata rehema ya kusamehewa dhambi zetu, na kupata wokovu au kuwezeshwa kuurithi ufalme wa mbinguni [MITHALI 28:13; LUKA 1:77].
MASKINI NI MTU ASIYEJIWEZA: Tukisema tunajiweza, tunapoteza nafasi yetu ya kuingia
mbinguni. Tukisema tunaweza kushinda dhambi kwa nguvu zetu wenyewe, au tunaweza kufanya lolote lile jingine kwa uwezo wetu; hali hiyo inatufanya tujione matajiri wa kiroho. Lakini, maskini, ni mtu asiyejiweza, na ndivyo itupasavyo kuwa. Pasipo Yesu Kristo, sisi HATUWEZI kufanya NENO LOLOTE hata lile lililo dogo kiasi gani [YOHANA 15:5; WAFILIPI 4:13]. Ili tupate kushinda dhambi, hatuna budi kwanza kupokea UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu [YOHANA 1:12]. Tukienda kwa Yesu kama maskini wasiojiweza, atatupa uwezo wa kushinda dhambi na uwezo wa kufanya mapenzi yake kila siku.
MASKINI, HANA AIBU: Maskini, utawakuta wakipita mitaani na kuomba hadharani, huku wakikiri waziwazi mbele ya watu kwamba wao ni maskini. Ndivyo itupasavyo kuwa tukitaka kuingia mbinguni. Hatuna budi kumkiri Yesu mbele ya watu na kumwambia kwamba sisi ni maskini, wenye dhambi na kuwa tayari kumwomba msamaha. Tusipofanya hivyo, tunakuwa siyo maskini wa roho, na hivyo tunakuwa na hatari ya kukosa ufalme wa mbinguni [LUKA 9:26; MATHAYO 10:32 ].
MASKINI, NI OMBAOMBA: Sisi nasi ikiwa ni maskini wa roho, hatuna budi kuwa ombaomba.
Tunaelekezwa, “Kuomba bila kukoma” [1 WATHESALONIKE 5:17]. Tunaanza kwa kuomba msamaha wa dhambi, na baada ya hapo, tukiisha kuokolewa, tunadumu kuomba ili tusiingie majaribuni [MATHAYO 26:41]. Tukiwa tunaruhusu siku ipite, bila maombi; basi tujue tumekwisha kuwa matajiri wa roho, na mbingu tunazifanya kuwa mbali nasi. Bwana atupe kila siku maisha ya kuomba bila kukoma!
S0MO: MAVAZI YA KIKAHABA
MITHALI 7:10
“Na tazama, mwanamke akamkuta ana mavazi ya kikahaba”. Kwa muda mrefu, katika kanisa la Mungu duniani, wakristo wengi wamegubikwa na utata mwingi kuhusiana na somo la mavazi. Maswali yafuatayo yamekuwa yakiulizwa bila kupata majibu sahihi:-
Je, mkristo anaweza kuvaa vazi lolote alipendalo?
Je, Mungu anaangalia moyo tu na haangalii mambo ya nje kama mavazi?
Katika somo hili la mavazi ya kikahaba lililojaa wingi wa mafunuo ya kipekee, unaweza kupata majibu ya maswali haya na mengi mengine; kwa kina, mapana, marefu, kwa ufasaha mkubwa. Katika somo hili utapata maarifa ambayo kila mtu anayeokolewa anapaswa ayapate katika uchanga wake wa kiroho ili aweze kuwa tofauti na watu wa dunia (mataifa). Ili aweze kuwa nuru au barua inayosomeka vizuri tofauti na jinsi alivyokuwa mwanzo kabla hajaokolewa (MATHAYO 5:16; 2WAKORINTHO 3:2-3).
Siku hizi za mwisho, tumekuwa na walimu wengi katika kanisa la Mungu ambao hufundisha kuwa Mkristo anaweza kuvaa vyovyote vile kwa hoja mbalimbali. Kabla hatujaziangalia hoja zao, hatuna budi kufahamu hili kwanza. Mungu ametahadharisha juu ya kuwepo kwa walimu wengi wa uongo. Kumbuka neno WENGI (2 PETRO 2:1-3; MATHAYO 24:11). Hukumu ya walimu wa uongo itakuwa kubwa sana ( YAKOBO 3:1). Hatuna budi kujua kuwa wote tutahukumiwa sawasawa na injili ya Paulo mtume (WARUMI 2;16). Paulo mtume anasema, injli inayohubiriwa kinyume na injili yake ni injli ya namna nyingine (WAGALATIA 1:6-9).Yeyote anayehubiri injili kinyume na injili ya Paulo mtume amelaaniwa na hawezi kuingia mbinguni (MATHAYO 25:41).Tukijua kuwa tumezungukwa na upepo wa elimu ya uongo (WAEFESO 4:14), tunapaswa kuchunguza maandiko kwa umakini. Watu wa Beroya, waliyachunguza maandiko kuona kama ndivyo yalivyo wakati Paulo na Sila walipokuwa wakiwafundisha (MATENDO 17:10-11). Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli (2WAKORINTHO 13:8). Kweli ni Neno la Mungu (YOHANA 17;17). Zifuatazo ni hoja za baadhi ya walimu wanaofundisha Neno la Mungu:-
HOJA YA KWANZA
Mungu haangalii mambo ya nje, anaangalia mambo ya ndani. Wanafundisha wakisema mavazi hayawezi kumzuia mtu kuingia mbanguni. Wanawatia moyo watu waendelee kuvaa mavazi wapendavyo bila kuangalia maandiko yanavyosema
Tunapaswa kujua kuwa utakatifu ni mwili na roho siyo ndani tu kama wao wasemavyo (1 WAKORINTHO 7:34; 2 WAKORINTHO7:1; 1WATHESALONIKE 5:23). Bwana Yesu alifundisha juu ya utakatifu kwamba unaanzia ndani na kasha nje. Hapo ndipo tunakuwa tumeutimizav utakatifu mwili na roho (MATHAYO 23:25-26). Yesu alisema “tutawatambua kwa matunda yao” (MATHAYO 7:15-21).Mtihutambulika kwa matunda yake. Matunda hayakai ndani ya mti, huwa nje ya mti. Hivyo, mavazi yanaweza kumtambulisha mtu, yeye ni nani na kazi yake ni ipi. Hata kwa kahaba ni hivyo (MITHALI 7:10).
HOJA YA PILI
Tuko huru ndani ya Yesu. Palipo na roho wa Mungu ndipo penye uhuru (WAGALATIA 5:1; 2WAKORINTHO 3;17). Hatuna budi kujua, kabla hatujaokolewa tulikuwa watumwa (YOHANA 8:33-36). Anachozungumzia Yesu ni uhuru mbali na dhambi (WARUMI 6:16-18). Baada ya kuokolewa sisi tunakuwa watumwa wa haki. Kwa hiyo, uhuru unaozungumziwa siyo wa kuvaa chochote au wa kufanya chochote kinyume cha Neno la Mungu.
HOJA YA TATU
Hatuko chini ya sheria wakati huu wa neema. Hatuna budi kufahamu kuwa, dhambi ni uasi wa sheria. Bila kuiasi sheria wewe si mwenye dhambi(1 YOHANA 3:4). Walimu hao, hutumia maandiko haya (WAGALATIA 5:4-5; ; WARUMI 6:14; WAGALATIA 5:18). Tunapaswa kufahamu kuwa, tumeokolewa na kutoka katika sheria ya Musa (WAEBRANIA 10:28). Hii ndio huitwa kongwa la utumwa. Tumetolewa kuwa chini ya sheria ya Musa na kuwekwa chini ya sheria ya Kristo (WAGALATIA 6:2). Sharia ya Kristo ni ngumu kuliko sheria ya Musa (MATHAYO 5:27-44). Sheria ya Yesu ni sheria ya Kifalme (YAKOBO 2:8). Sheria ya kifalme siyo ya kuchezea. Mfalme akiagiza jambo hana mjadala.
HOJA YA NNE
Tuvae vyovyote ili tuwapate na mataifa. Walimu h
ao wanaamua kushusha viwango na kujaribu kurahisisha njia ya kwenda mbi
nguni(1 WAKORINTHO 3:11). Msingi umekwisha kuwekwa ambao ni Yesu Kristo. Yesu ni mchungaji mkuu, wachungaji wote wako chini ya mchungaji huyo. Wachungaji wanapaswa kujifunza kwa mchungaji mkuu Yesu Kristo (WAEBRANIA 13:20). Alionesha kielelezo kwa kutokushusha viwangop vya mafundisho ili kuwa na idadi kubwa ya washirika (YOHANA 6:61, 66-68). Wengi miongoni mwa wanafunzi wake walirejea nyuma na wasiambatane naye ( Yesu ) tena. Kilichowafanya kukwazika ni mafundisho magumu kutendea kazi ( Neno gumu ). Yesu kristo ili kuonesha mfano kwa wachungaji wa sasa, yeye hakuchuja Neno lake ili waendelee kuwepo bali hata wale wachache (tenashara/mitume) aliwageukia na kuwauliza kama na wao wanataka kuondoka..Alikuwa tayari kubaki peke yake na kuanza kazi upya. Tunaweza kuwa na orodha ndefu ya majina ya washirika waliojiandikisha kanisani lakini majina hayo yakawa hayapo katika kitabu cha majina ya Mungu (kitabu cha uzima). Hatuwezi kuwaingiza watu mbinguni kwa viwango vyetu wenyewe, ni kwa kuongozwa na Neno la Mungu tu.
Wakitoka ndipo tunapojua kuwa hawakuwa wa kwetun(1 YOHANA 2:19). Sharti kanisa liongezeke kwa watu wanaookolewa na si vinginevyo (MATENDO 2:47). Mtu aliyeokolewa, amri za Mungu siyo nzito kwake (1YOHANA 5:1-5). Tunapaswa kujua kuwa watakaoingia mbinguni hawatakuwa wengi ukilinganisha na watakaotupwa motoni (MATHAYO 7: 13-14). Mataifa watutambua kuwa tumeokoka kwa matendo yetu (1 PETRO 2:12; 2WAKORINTHO 3:1-3; MATHAYO 26:69-73).
MOYO WA SOMO
MAVAZI YA KIKAHABA (MITHALI 7:10)
Ujira au mshahara wa kahaba na hanithi hautakiwi kupokewa ndani ya nyumba ya Mungu (Torati 23:17-18). Kama biblia inataja juu ya kuwepo kwa mavazi ya kikahaba, hatutakiwi kupuuzia.. Mtu akiokoka anapaswa kubadilika kwa kuyafanya matendo yanayoambatana na kutubu kwake (MATENDO 26:20). Tunapaswa kuzaa matunda na yaonekane (MATHAYO 3:8). Tukikosa ushuhuda mzuri, tunawafungia wengine kuingia katika ufalme (MATHAYO 23:13). Watu wanaookoka wanatoka katika mazingira na hali tofauti hivyo tunatakiwa kuwafundisha ili waishi sawa na viwango vya Neno la Mungu. Pia desturi na tamaduni zetu zinaweza kuwa kinyume na Neno la Mungu kwa sababu waanzilishi wake wengine hawajaokoka. Neno linasema tusifuate nasaba zisizo na ukomo. Nasaba ina maanisha tamaduni. (1 TIMOTHEO 1:3-4). Mavazi ya kikahaba yanakuwa na lengo la kuwavuta hao tunaotaka kufanya nao uchafu.
Ifuatayo ni misingi inayotupa kujua mavazi ya kikahaba.
MSINGI WA KWANZA
HATUTAKIWI KUBADILI MATUMIZI YA ASILI.
Mungu anasema katika Neno lake “wala msimpe Ibilisi nafasi” (WAEFESO 4:27). M,apepo yana uwezo wa kufanya uzinzi au uasherati na binadamu. Yanaweza kuja kwa namna mbalimbali (WALAWI 17:7). Waathirika wakubwa wa nguvu za giza (mapepo na majini ) ni wanawake na mgogoro mkubwa ni kwenye mavazi ya kikahaba. Mavazi ya kikahaba ni mlango mkubwa wa mashetani kuwashambulia watu. Kubadili matumizi ya asili ya viungo vya binadamu yawe yasiyo ya asili nyuma yake kuna mashetani. Tukifanya hivyo tutakuwa tunampa nafasi Ibilisi (MWANZO 19:1-28; YUDA 1:6-8). Wakati wa Ruthu katika mji wa Sodoma na Gomora na miji jirani, walifanya uchafu wa kila namna wanaume na wanawake wakiwakiana tama lakini nyuma yake yalikuwepo mashetani (YUDA 1:6-8) “Wakaendelea kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili”. Kumbe kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili nyuma yake kuna mashetani. Kazi ya shetani ni kuharibu mpango wa Mungu wa uumbaji, mpango wa Mungu wa maumbile (YOHANA 10:10). Mtu akipagawa na mashetani ndipo anaanza kuharibu mpango wa Mungu kwa kufanya mambo yasiyo ya asili (MARKO 5:1-20; WARUMI 1:26-28). “Mungu akaona kila alichokifanya (kiumba) na tazama ni chema (kizuri) [MWANZO 1:31]. Shetani anatupandikizia mawazo mabaya tuone kuwa Mungu alikosea katika uumbaji wake. Anatufanya tuone nywele za wazungu ni nzuri sana kuliko zetu waafrika. Pia anatufanya tuone rangi ya ngozi yao ni nzuri kuliko yetu hii nyeusi n.k. Kufanya kinyume na uumbaj
i wa Mungu wa maumbile yetu ni kumsahihisha Mungu. Kiumbe kinamuona y
eye aliyekiumba hana ufahamu. Kitendo hicho ni sawa na kutaka kumpindua Mungu kwenye kiti chake cha enzi. Ni dharau ya hali ya juu (ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21). Ujasiri wa kumdharau Mungu unatoka wapi? Bila shaka unatoka kwa shetani. Mungu anasema “Wao wanaoniheshimu nitawaheshimu na wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu (1 SAMWELI 2:30).
Mpango wa Mungu kwa kanisa unaweza kuondolewa na mashetani yakatawala kabisa. Mambo yanayofanywa yasiyo ya asili ni haya yafuatayo:-
1. WIGS / WIGI
Hizi ni nywele zinazovaliwa na wanawake na wanaume kwa idadi ndogo.Zipo aina mbili za nywele za bandia.
(a). Synthetic wigs and (b). Human hair wigs
A. SYNTHETIC WIGS (Nywele za bandia)
Ni mawigi yanayotengenezwa zaidi kwa nyuzi za naironi.Yapo material yanayotumika katika utengenezaji wa aina hiyo ya mawigi..
Watengenezaji wa mawigi wanaeleza kwamba ni kwa nini watu wanavaa wigi.
Ingia katika tovuti ifuatayo ya watengenezaji wa nywele za bandia uone mengi sana.
WWW.bald-hairloss.com/Whaat-Are-The-Types-Of-Hair-Wigs-And-How-To-Use-Them/ ENGLISH
“Today’s market is full of wigs for those who wish to get over their inferiority complex having this hair or bald matches and those who wish to look confident as ever even with a baldness/hair fall disorder”. SWAHILI
“Soko la leo duniani limejaa wigi kwa ajili ya watu wanaojiona duni na kwa ajili ya watu wenye vipara na ambao nyele zao hazikuota vizuri ili na wao waonekane wenye nywele”
WHAT SYNTHETIC WIGS ARE MADE FROM?
WWW.wigsguru.com or / Synthetic.wigs.html
“Synthetic wigs are not made from human hair, what are they made from? There are several common material that found in synthetic wigs, of course many of these wigs are made primarily nylon. Dynel and acetate fibers are also used they can be others as well”.
B. HUMAN HAIR WIGS
(Wigi zinazotokana na nywele za binadamu)
Wigi za namna hii hutokana na nywele za wahindi ingawa kwa asilimia ndogo hutokana pia na nywele za wazungu.Nywele za wazungu zinakatika haraka (si laini) lakini nywele za wahindi ni laini.
Nywele hizi za wahindi zinatoka katika hekelu moja maarufu la kihindi.Wahindi ni waabudu miungu.Pamoja na kuwepo miungu wengi lakini lipo hakalu moja ambalo wanamwabudu mungu mmoja anayeitwa Vishnu. Hili hekelu liko India katika eneo linaloitwa mji:Tirupati,wilaya: Chittoor, Jimbo: Andura Pradesh.Hekalu hili liko eneo la kusini katika jimbo hilo.Jina maarufu la hekalu ni TIRUMALA TIRUPATI DEVASTHANAMS (Venkateshwara Temple).Mungu wao ni VISHNU (Lord Balaji) kwa namna ileile ya LORD JESUS (Bwana Yesu).Unaweza kuliona hekalu hilo katika tovuti hii: WWW.tirumala.org, pia WWW.madrasi.info/tirupati.jpo,
Unaweza kuona habari nyingi sana za hekalu hilo pamoja na jinsi nywele zinavyotolewa sadaka.Wanaeleza katika mtandao wao kuwa ,wametaajirika sana kutokana na sadaka za nywele ambazo baadaye zinatengenezwa wigi (human hair wigs) ambazo huuzwa kwa watu wanaojiona duni katika miili yao.Wanaeleza kuwa mtu akivaa wigi hizo anaonekana kama dori,Tovuti yenyewe ni hii:-
WWW.hindu.blog.com/2007/06/on-human-hair-tonsured-at-tirumala.html
Wanaeleza kuwa kwa mwaka mzima watu wanaokwenda hekaluni hapo ni milioni ishirini na hawa wote wanatoa sadaka ya nywele zao kwa kunyolewa hekaluni hapo.
Katika ibada zao kwa huyo mungu wao,ili kuamini kuwa amejibu maombi yao,wanatoa sadaka ya nywele zao kama sadaka ya shukrani.Kwasababu hiyo kuna mamia ya vinyozi ambao wameajiriwa kwa kazi hiyo.Kwa siku moja nwananyolewa watu 1500.Ni hekalu tajiri sana kuliko mahekalu mengine ya miungu na linakuwa bisy wakatiwote.
WWW.hindu.blog.com/2007/06/human-hair-tonsured-at-tirumala.html
“The Temple at Tirupati is one of India’s busiest .The Temple has invigorating business selling hair. Many of the Temples 20 millions visitors each year shave their hairs in gratitude for a blessings.
The human hair from Hindu Temples like Tirupati is nicknamed “Temple Hair” and is
of great demand due to its spiritual value.
Kwa maelezo zaidi angal
ia katika tovuti ya hekaru iliyoko hapo juu .
2. KUBADILI ASILI YA NYWELE.
Je, unafahamu collagen ni kitu gain, na kinapatikana wapi?
COLLAGEN ni seli nyororo ambayo inanata kama mpira ambayo inatokana na tishu zilizoungana. Collagen nyingi zinatokana na placenta au kondo la nyuma la uzazi. Mtoto anapokuwa katika tumbo la uzazi kunakuwa na tishu zinazomuunganisha motto na mama.. Kutokana na mtafitin mashuhuli anayeitwa Dr. Olga Fairfax unaweza kusoma habari zake katika mtandao ufuatao:- WWW.skepticfiles.com/mys2/deadbaby.html
Tafiti zake zinaonesha nchini Marekani mamba 1,500,000 hutolewa kila mwaka na kuuzwa katika hospitali kadhaa huko Marekani. Makampuni yanayotengeneza vipodozi huko nchinin Marekeni, hununua Collagen inayotokana na mamba hizo. Unaweza kuona mengi kuhusiana na Collagen kwa kwa kuingia kwenye mtandao kwa kutumia (keyword) ufunguo huu “ COLLAGEN FROM HUMAN PLACENTA HAIR PRODUCTS”. Mfano wa vipodozi vinavyotokana na placenta ni vile vyenye maneno “PLACENTA PLUS SHAMPOO au PLACENTA ASSENCE”. Unaweza kuingia kwenye mtandao ukaona kwa kina WWW.broadwaybeaties.com. Katika mtandao ufuatao unaweza kuona baadhi ya vipodozi vyenye Collagen ndani yake. WWW.beoti.eu/products.html.
Vipodozi vingine mbali na hivyo vyenye Collagen, huwa na kemikali kali sana kama vile ZEBAKI (Mercury). Zebaki ina tabia ya kupenya na kuingia mwilini kwa kupitia matundu ya vinyweleo vya mwili. Madhara yake ni makubwa sana. Ni muhimu kufahamu kuwa Zebaki hutumika kusafishia madini katika machimbo mbalimbali. Wachimbaji wa madini hulazika kuvaa gloves ( mipira ) wakati wa kusafisha madini ili kuepukana na madhara ambayo yangetokea kama wangetumia Zebaki bila kuvaa mipira.
Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayosababishwa na kutumia vipodozi vyenye kemikali ya Zebaki;- 1. Huua nywele kabisa. Nywele za mtu hufa kabisa na ndiyo maana inakuwa rahisi
kuzilaza upande wowote. katika
2. Inaweza kusababisha ugumba kwa mwanamke. Inaweza kusababisha uvimbe katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na kufanya seviksi kushindwa kufunguka wakati wa tendo la ndoa.
3. Inaweza kusababisha saratani ( kansa ) ya ngozi.
4. Inasababisha mtu kupata mvi kabla ya wakati wake.
5. Nyele hazioti vizuri, wakati mwingine inaweza kusababisha kuwa na kipara . Zebaki inaua seli za mwili zinazowe zesha nywele kuota.
3. KUBADILI RANGI YA NGOZI.
( Kujichubua)
Mungu anaumba ngozi kwa makusudi yake na mazingira yake. Mingu anauliza, “Je mwafrika anaweza kubadili rangi ya ngozi yake?’. Lakini mwafrika anamjibu Mungu kwa dharau eti tunaweza. (YEREMIA 13;23; 1 SAMWELI 2;30).Kitendo cha kuchubua ngozi kwa lengo la kutaka kuwa mweupe ni kumdhyaarau Mungu (muumba). Mkushi anayezungumziwa katika YEREMIA 13:23 ni mtu wa Libya katika bara la Afrika. Kushi ilikuwa sehemu ya Libya. Mungu anasema weusi ni uzuri (WIMBO ULIOBORA 1:15). Kitaalamu katika ngozi kuna chembechembe ambayo kazi yake ni kuzuia sumu ya mionzi ya jua. Chembechembe hizi zinaitwa MELANINI. Kadri seli hizi zinavyokuwa nyingi zaidi ndani ya mtu ndivyo anakuwa mweusi zaidi. Mungu aliweka seli hizi kwa wingi kwa waafrika kulingana na mazingira. Jua linawaka sana katika mazingira ya Afrika kuliko sehemu zingine, hii ni kwasababu tuko karibu sana na mstariwa Ikweta. Tupo katikati ya dunia.
Katika kutafuta weupe kwa watu wanaojiona duni na kumdharau Mungu (Muumba) aliyewaumba, hutumia krimu (crème), loshen na sabuni zenye viambata vya sumu kuua seli za MELANINI. Viambata hivyo ni Hydroquinone na Mercury (Zebaki). Sumu ambazo hutumika kuua seli za Melanini ni kama :-
1. BITHONOL. 2. STROIDS 3. HYDROQUINONE 4.MERCURY
(Zebaki) 5. HEXACHLOROPHENE 6. ZIRCONIUM 7. VINYLCHLORIDE
8. HALIGENATED SALICYLANILIDES 9. CHLOROQUINONE
10.CHLOROFORM 11. METHYLENECHLORIDE 12. AEROSOL
12.CHLOROFLUORO CA
RBONS PROPELLANTS
Ndani ya vipodozi mbalimbali huwa kuna su
mu hizo (kemikali) kwa ajili ya watu wanaojiona duni. Vitu vingine vinavyotumika ni pamoja na mafuta ya transfoma, maji ya betri, vidonge na sindano. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya madawa hayo:-
Ngozi kuwa na mabakamabaka.Kuwa na vipele au uvimbevimbe usoni.
3 Mwasho kwenye ubongo.
Saratani (kansa) ya damu, ngozi, figo, n.k.Kuzaa mtoto wenye mtindio wa udongo.
Mwili ni hekalu la Mungu, tusiufanye kuwa maskani ya Mashetani
(1WAKORINTHO 3:16-17; UFUNUO 18:2-3)
4. TEETH GRILLS
(Grili za meno)
Haya ni meno yanayotengenezwa kwa madini ya thamani. Ukiingia katika mitandao ifuatayo ya internet, uaona hayo meno ya bandia yakitajwa kuvaliwa na makahaba
WWW.iceddouigear.com/grillz-gold-teeth.php. Neno PIMP linazungumzia mtu anayefanya kazi ya kuwaajiri makahaba katika kampuni, kwa shughuli ya ukahaba akilipwa ujira wake na wateja wanaokuja kufanya naye uchafu. Maana ya neno PIMP unaweza kuiona katika mtandao ufuatao:-WWW.en.wikipedia.org/wiki/pimp. Ni jambo la kushangaza mpendwa kuvaa meno ya bandia na huku ana meno ya asiliya Mungu.
5. ARTIFICIAL FINGER NAILS
(Kucha za bandia)
Ni kucha za bandia ambazo hubandkwa kwa gundi katika vidole. Waru wanaovaa kucha za bandia , wanafunika kucha za asili kwa kucha za bandia.. Unaweza kuona aina ya kucha za bandia katika mtandao ufuatao:- WWW.sisegeek.com/What-are-thedifferent-types-of artificial-finger nails.
6. FALSE EYE LASHES
(Nyusi za Bandia)
Baba wa uongo shetani ametengeneza nyusi za uongo na watu wanavaa. Watu wanakwangua nyusi zote za asili na kutia nyusi za uongo. Wengine wanabandika juu ya nyusi za asili. Unaweza kuona aina ya nyusi za bandia katika mtandao ufuatao. WWW.wigsgumi.coni.com.au/false-eyelashes.html. Nia yake mtu anayebandika nyusi za bandia si nzuri na ni kazi ya shetani.
MSINGI WA PILI.
MAVAZI NI YA KUFICHA UCHI.
Mungu ndiye mwanzilishi wa mavazi (MWANZO 3:7). Lengo la kuvaa mavazi ni kuficha uchi (kujisitiri) MWANZO 3:21. Zipo sehemu katika mwili ambazo zinaitwa sehemu za siri. Binadamu ameumbwa na soni au aibu, kwa hiyo katika hali ya kawaida hawezi kukubali sehemu zake za siri zionekane. Mtu akipagawa na mapepo ndipo anaweza kuwa uchi na kwake likawa ni jambo la kawaida. Tunamuona mtu aliyepagawa na mapepo hadi yakamfanya kuwa uchi maisha yake yote bila aibu (MARKO 5:1-20). Mtu akipagawa na mapepo hawi na aibu kamwe (MARKO 5:15). Kwa mfano, katika huduma za maombezi utaona mapepo yakitaka kufanya mwanamke kukaa uchi nah ii ndo kazi ya kwanza ya mapepo. Na mwanamke huyo hawezi kuona aibu katika hali hiyo. Ndiyo maana wanatakiwa kuwepo wanawake wenzake wa kuhakikisha mwanamke mwenzao hakai au hawi uchi.
Viwango vya kutamani (tama) vya mwanamke viko chini kuliko vya mwnaume (MWANZO 3:16). Ndiyo maana mwanaume ndiye anayetakiwa kumtafuta msaidizi. Mke ni msaidizi, mume amepewa kumtawala. Siku zote bosi humtafuta msaidizi na siyo msaidizi anayemtafuta bosi.. Matamanio ya mwanamke wakatio mwingine yanahitaji kuamshwa (WIMBO ULIO BORA 2:7). Biashara ya ukahaba ikifanya na wanaume haiwezi kupata wateja kwasababu wanawake matamanio yao yako chini. (EZEKIELI 16:33-34). Katika mpango wa Mungu sasa, mwanamke anatakiwa kumlinda mwanaume (YEREMIA 31:22). Kwasababu viwango vya matamanio vya wanaume viko juu, wanawake wanapaswa kuwalinda wanaume ( wasiwakoseshe ). Wanawake hawapaswi kuvaa mavazi ya kuwakosesha wanaume (MATHAYO 18:6-7). Ukileta jambo la kukosesha na kumkosesha mtu, Yesu anasema “alejaye jambo la kukosesha atatupwa katika kilindi cha bahari ya moto. Uchi wa mwanamke unaanzia kwenye goti (magoti) kuelekea juu mpaka kwenye mifupa ya kifuani maeneo ya shingo. Wakati huu wa kanisa mwanamke hatakiwi kuwa kama Hawa aliyetumiwa na Shetani kumwangusha mwanaume Adamu. Wakati wa Yesu, mwanamke ndiye aliyekuwa wa kwanza kumwinua Yesu. Yafuatayo yasifanywe, vinginevyo hatutakuwa na tofauti na makahaba (MITHALI 7:10).
Kuvaa mavazi yanayoonesha mstari unaotenganisha matiti.
Kuonesha matiti kwa namna yoyote.Kuonesha tumbo na kitovu.Kuonesh
a maungo yetu kwa kuvaa nguo zinazobana.Kuvaa nguo zinazoonesha nguo zetu za ndani (Transparent).Kuacha mgongo wazi.Kuvaa taulo kwa wanaume na kuacha tumbo wazi mbele ya wanawake.Kuacha kifua wazi kwa wanaumeWanaume kuvaa bukta mbele ya wanawake.Kuacha makwapa wazi.Wanawake kuvaa nguo fupi na zenye mpasuo.
Wanawake wanatakiwa kuvaa mavazi ya kusitiri kabisa mwili wao (1 TIMOTHEO 2;9). Kwa wanaume inakuwa mgogoro mkubwa wanapoona sehemu za siri za mwanamke.
MSINGI WA TATU
MWANAMKE HANA BUDI KUVAA MAVAZI YA KIKE NA MWANAUME MAVAZI YA KIUME
KUMBUKUMBU LA TORATI 22:5
“Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi yampasayo mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, MUNGU wako”. Tusipopata maarifa ya kutosha kuhusiana na mavzi anayotakiwa kuvaa mtu aliyeokoka, tunaweza kuwa tunafanya MACHUKIZO mbele za MUNGU pasipo kujua.
Ili kujua mavazi yanayostahili, Mungu anasema “maumbile yetu yatufundishe” (1 WAKORINTHO 11:14). Mpaka katika suala la mavazi aliuweka Mungu mwenyewe. (KUMBUKUMBU 22:5). Maumbile ya mwanamke na mwanaume yanatofautiana. Mitindo ya nguo inakuja kutokana na maumbile yetu. Suruali inatakiwa kuvaliwa na wanaume nah ii ni kibiblia kabisa. Hatuoni katika biblia sehemu ambayo inataja suruali kuvaliwa na mwanamke. Tunaona biblia ikiwataja wanaume wakiwa wamevaa suruali (KUTOKA 39:27-28; WALAWI 16:3-4; EZEKIELI 44:15-18; DANIELI 3:20-21, 26-27). Nguo zingine hazikutajwa katika biblia kama ilivyotajwa suruali hii ni kwa sababu wakati wa biblia hazikuwepo hizo nguo. Lakini jambo la kuzingatia ni maumbile, yanapaswa kutufundisha.. Baada ya kuokoka, hatupaswi kuongozwa na desturi na tamaduni kinyume na Neno la Mungu. (I TIMOTHEO 1:3-4). Neno NASABA linazungumzia mambo ya jadi na ukoo. Mambo ya jadi na ukoo hatutakiwi kuyajenga kama msingi wa wetu. Mkristo anajenga msingi wake kwenye Neno la Mungu (ZABURI 119:105; ZABURI 119:9)
Ni muhimu kujua kuwa, katika nchi zingine mila na desturi zao ziko kinyume na msingi wetu wa ukristo. Waanzilishi wengine wa mila na desturi hawajaokolewa hivyo hawawezi kufuata Neno la Mungu na ndiyo maana unaweza kukuta mila zetu na desturi zingine zinapingana na Neno la Mungu. Wengine bila kujua hutetea uvaaji wa suruali kwa kisingizio cha mila na desturi za mahali Fulani. Wengine wanasema mbona wazungu wengi wanawake wanavaa suruali, ina maana wote hao na wengine wengi watatupwa motoni kwa kosa hilo? Ni muhimu kufahamu kuwa uwingi wa watenda dhambi kwa Mungu si hoja kabisa. Wakati wa Nuhu, Mungu aliangamiza dunia nzima akawaacha watu wanane tu waliokuwa wakiishi katika mapenzi yake (MWANZO 6, 7 ) sura zote. Pia wakati wa Ruthu, Mungu aliwateketeza watu wote katika miji ile isipokuwa watu watatu tu katika miji ile waliolifuata Neno lake na kuwa kinyume na mkutano uliokuwa ukitenda dhambi (MWANZO 19:1-28). Mungu anasema, “ usiandamane na mkutano kutenda uovu” (KUTOKA 23:2). Lengo la kuvaa suruali na kuzitetea ni nini? Wakristo tunatafuta kupeza kwa nani? Tunatafuta kumpendeza Mungu na si vinginevyo (ZABURI 73:25; WAGALATIA 1:10). Tunatakiwa kukubaliana na kuitwa wajina na washamba katika mambo maovu (WARUMI 16:19-20). Wengine wanasema tunatakiwa kwenda kisasa. Ni muhimu kujua kuwa biblia haifanyiwi (revision) mapitio mapya Neno la Mungu haliwezi kubadilika kwa namna yoyote ile. Mungu anasema tufuate mapito ya zamani (YEREMIA 6:16; AYUBU 8:8). Kutafuta, kuuliza habari za mapito ya zamani ambayo hata wanafunzi wa Yesu waliishi katika viwango hivyo bila kuangalia dunia iko katika hali gain. Wanafunzi wa Yesu, walionekana washamba, watu waliopitwa na wakati, watu duni, walionekana kuwa adui wa jamii za nyakati zile kwa sababu ya viwango vyao vya utakatifu. Tunaweza kuthibitisha hayo katika biblia ifuatayo:-
[Thompson Chain-Reference Bible (ARCHAELOGICAL SUPPLEMENT) Page 1688 Topic No. 4428 Topic Heading ROME] Inasema, “The Christian were changed with being unsocial and odd and came to be hated a
nd counted as enemies of society. They were simple and modest i
n dress, strictly moral in their conduct and would not go to the games and feasts. Some Christian even condemmed those who sold fodder for the animalsto be sacrificed to pagan gots. Kitabu hiki kinapatikana hata katika nchi yetu ya Tanzania. Wakristo walionekana kuwa adui wa jamii, hawakuwa na mchezo katika maadili yao. Hawakufanya mchezo na maandiko kwa visingizio vya ukisasa (kwenda na wakati). Siku zote walidumu katika Neno bila kuchuja viwango.
MSINGI WA NNE
MAANDISHI KATIKA MAVAZI YAWE YA KUMTUKUZA MUNGU
(KUMBUKUMBU LA TORATI 11:18-21)
Maneno ya Mungu ndiyo yanayokuwa maandishi katika nguo zetu. Maandishi yanayokuwa katika nguo zetu, yanakuwa na maana, yanazungumza kabisa. Nguo zingine za wanawake zinakuwa na maandishi yasiyomtukuza Mungu. Mfano Kanga. Kanga zinakuwa na maneno ya lugha ya Pwani, lugha zingine ni za kikahaba. Unaweza kuvaa nguo yenye maana nyingine kwa ajili ya tukio maalum. Mfano sherehe za uhuru n.k.Biblia inasema, “mtukuzeni Mungu katika miili yenu”. Kuvaa nguo zenye namba ni makosa. Unapaswa kujiuliza namba hiyo ni ya nini? Mapepo nayo yana namba. Milio ya simu na saa yote inapaswa kumtukuza Mungu. Michoro ya aina yoyote katika miili yetu hairuhusiwi (WALAWI 19:28). Michoro ya tattoo katika miili yetu hairuhusiwi, ni machukizo kwa BWANA. Neno tatoo linapatikana katika biblia ya kiingereza ya tafsiri ya New International Vision katika (LEVITICUS 19:28).
MSINGI WA TANO
MAVAZI HAYANA BUDI KUWATOFAUTISHA WAKRISTO NA MATAIFA
(WARUMI 12:2; WAEFESO 4:17).
Yako mavazi ambayo hata katika sheria za serikali yatakuwa hayaruhusiwi kuvaliwa kwa sababu yanamfanya mtu kuonekana kama mhuni. Kama kwa mataifa ni mavazi ya kihuni kwatu sisi tuliookoka (nuru ya ulimwengu) yawezaje kuwa mavazi ya adabu? Haki yenu isipozidi haki ya mafarisayo hamtaingia mbinguni (MATHAYO 5:20). Mavazi kama jinzi, kadeti yote haya ni mavazi ya kihuni. Bungeni na kwenye ofisi za serikali mavazi hayo hayaruhusiwi kuvaliwa kabisa. Jeshini na katika sahemu mbalimbali watu hawaruhusiwi kufuga ndevu. Hata kama sheria haitaji ndevu, tunapaswa kuwa na sheria hiyo (1 WAKORINTHO9:20). Unyoaji wa nywele uwe katika utakatifu wote. Mapanki ya aina zote kwa watu waliookoka hayatakiwi. Uvaaji wa kofia za kuficha sura hautakiwi. Mungu anaangalia nia yako (WARUMI 12:2; WAEFESO 4:17).
MSINGI WA SITA
MAPAMBO YOTE HAYATAKIWI
(1TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3:3-5)
“Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri; pamoja na adabu nzuri; na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele , wala kwa dhahabu n
A lulu, wala kwa nguo za dhamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu” (1TIMOTHEO 2:9-10). “kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele, na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo na dhamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao” (1 PETRO 3:3-5).Tunaona kuwa , wanawake watakatifu wa zamani nao hawakujipamba kwa mapambo yaharibikayo, walijipamba kwa mapambo ya rohoni. Mapambo ya aina yoyote hayatakiwi katika miili yetu. Wapo watu wanaofundisha juu ya kujipamba, nao wana hoja zao. Andiko wanalotumia katika kutetea ni hili (EZEKIELI 16:1-14). Andiko hili linazungumzia juu ya Yerusalemu. (EZEKIELI 16:14).Kinachozungumziwa hapa ni ukamilifu.
Unaweza kuona kupambwa kunafananishwa na mapambo ya mataifa lakini kiroho inazungumzia nini? “Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, huwapamba wenye upole kwa wokovu (ZABURI 149:4). “Mwanangu, ysikilize mafundisho ya baba yako, wala usiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichani pako, Na mkufu shingoni mwako” (MITHALI 1:8-9). Mafundisho na sheria vinatajwa kama mapambo ya kawaida ya mataifa. Mafundisho ya Neno la Mungu yanatupamba na kutufanya kuwa safi. Kinachozungumziwa hapa ni mapambo ya wokovu ambayo tunapambwa na Mungu (ISAYA 61:10) “ Nitafurahi sana
katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maa
na amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu”. Mapambo yanavaliwa na mataifa, watu wasiomjua Mungu na ndiyo maana Mungu anawakataza watu wake kuvaa mapambo (1 PETRO 3:2-5; 1 TIMOTHEO 2:9-10). Mungu anasema “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele na kujitia dhahabu na kuvalia mavazi”. Hapa kinachozungumziwa ni mapambo, mavazi yanayozungumziwa ni mavazi ya mapambo. “Bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika, yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo na thamani kuu mbele za Mungu”. Mungu anapendezwa na mapambo ya ndani (wokovu), tunaona hili katika (ZABURI 149:4; ISAYA 61:10). Katika maisha yote ya mwanadamu hapa duniani, Mungu hakuwahi kuruhusu mapambo kuvaliwa na watu wake. Tunaona wakati wa Yakobo Mungu aliwaambia Waisraeli waondoe miungu migeni waliyokuwa nayo (mapambo), ni mavazi ya kigeni kwa Waisraeli, si mavazi yao (MWANZO 35:1-5). Wakati wa nabii Musa Mungu alikataa kwenda kati yao hadi pale walipochukua hatua ya kuvua mapambo au vyombo vya uzuri (KUTOKA 33:4-6). Mungu hawezi kushuka katikati ya watu wenye machukizo mbele zake, lazima yaondolewe kwanza ndipo uwepo wa Mungu udhihirike. Machukizo ya namna hii yakiruhusiwa hatuwezi kuyaoanmatendo ya mitume maishani mwetu. Miujiza, ishara na maajabu waliyofanya Wakristo wa kanisa la kwanza kwetu yatakuwa katika maneno tu (nadharia) na si katika matendo. Ni muhimu kufahamu kuwa hata makuhani (wachungaji, walimu, wainjilisti, mitume na manabii) nao pia wanaweza kutenda dhambi na kuruhusu machukizo. Wanapofanya hivyo, mkono wa Bwana wa kuponya (miujiza) unaondolewa kwao, utabaki tu usanii wa miujiza midogo midogo (2 MAMBO YA NYAKATI 36:14-16). Mapambo ya mikufu na pete yanahusiana na ibada za mabaali (miungu) (HOSEA 2:13; MWANZO 35:1-5). Vyombo vya uzuri (mapambo) vinahusianishwa na uzinzi na uasherati., ni mavazi ya kikahaba (EZEKIELI 23:26-30, 40,42). Mungu anawauliza waisraeli, watafanyaje watakapotekwa na mataifa na kulazimishwa kujipamba kinyume na mpango wa Mungu? (YEREMIA 4:30). Wachungaji na walimu wengine wa Neno la Mungu, wanapenda kuzungumzia juu ya roho ya Yezebeli lakini wanashindwa kutambua kuwa kuruhusu mapambo kwa watu waliookoka ni roho hiyohiyo ya Yezebeli inayotenda kazi.(2 WAFALME 9:30-37). Yezebeli alikuwa mataifa, aliolewa na mfalme Ahabu wa Israeli, akaingiza ibada zao za mabaali (miungu) na mambo ya kujipamba, mambo ya kujitia wanja, , marangirangi yote ilikuwa ni kazi yake Yezebeli. Mungu anatuonya kutofuata mafundisho ya Yezebeli, mwanamke aliyehusudu mapambo (UFUNUO 2:20). Kwa hiyo, mafundisho yanayofundishwa yakitia moyo wanawake kuendelea kuvaa mapambo na kujitia rangi miili mwao ni mafundisho ya Yezebeli.
Tunaona baadhi ya mapambo yametajwa katika (ISAYA 3:16-24). Hatuna budi kuviangalia kwa undani ili tupate kujua ni vigani vinatajwa ambavyo havitakiwi kuvaliwa na mkristo.
(i). Viatu virefu sana havitakiwi. Lengo au nia yako ni nini?
(ii) Njuga
(iii) Pete za masikio (Heleni).
(iv) Vikuku (Mabangili)
(v) Taji
(vi) Dusumali (Namna fulani ya mapambo ya kichwa, vibanio vya nywele n..k).
(vii) Mafurungu (namna za mabangili zinazofanana na vikuku). Shanga zote hazitakiwi.
(viii) Vitambi (Namna ya mikanda ya kuvalia nguo ambayo inakuwa mikubwa sana kwa
Unene). Siyo makosa kuvaa mikanda (YEREMIA 13:1-2).
(ix) Matarasimu (Namna ya banbili zinazovaliwa mikononi kama saa lakini siyo saa).
Kuvaa saa kwa lengo la kukusaidia kujua muda siyo makosa.
(x) Vifuko ( kutembea na handbag au mfuko mkubwa sana ambao hauna kitu ndani. Vifuko vya namna hiyo havitakiwi.
(xi) Vioo vidogo, Hapa inazungumziwa miwani inayovaliwa kwa lengo baya. Mungu anaangalia nia ya ndani. Mfano kuvaa miwani myeusi ili usionekane lengo lake si zuri. Miwani ya kusomea au kuonea si tatizo.
(xii)Pete (ISAYA 3:21), Hapa zinazungumziwa pete zote zinazovaliwa mikononi. Ni muhimu kufahamu kuwa hak
una pete ya ndoa kibiblia. Ndoa ya kwanza ya Adamu na Eva ha
wakuvalishwa pete na Mungu wala wao kuvalishana (MWANZO 1:27-31). Hata sasa anayewaunganisha wana ndoa ni Mungu mwenyewe (MATHAYO 19:3-6). Je, ni kweli Isaka na Rebeka walivalishana pete ya ndoa kama wengine wasemavyo? Soma (MWANZO 24:29, 47), Katika andiko hilo ambalo ni andiko pekee wanalotumia kuhalalrisha uvaaji wa pete iitwayo ya ndoa, tunaona maneno “Vikuku na Hazama”.. Kwa hiyo tunapata kufahamu kuwa Rebeka alivalishwa vikuku (mabangili) na hazama (pete ya puani kwa sasa ni heleni ya puani).. Mbona hawavalishani puani sasa? Angalia maana ya hazama mwishoni mwa biblia kwenye maelezo ya maneno magumu. Pete imekatazwa kuvaliwa (ISAYA 3:21). Haya ni mapokeo ambayo yalianza kipindi kanisa lilikuwa katika wakatiza giza ambapo vitu vingi ambavyo ni mapokeo viliweza kuanzishwa na hata sasa tunaviona katika madhehebu ya makanisa yanayoitwa ya kikristo.
(xiii) Kusuka nywele (1 TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:2-6). Hatutakiwi kusuka nywele kwa namna yoyote. Wanawake wameruhusiwa kuwa na nywele ndefu lakini ziwe katika hali ya asili (1WAKORINTHO 11:13-14). Hapa tunajifunza kuwa mwanamke anapaswa kufunika kichwa wakati asalipo au anapohutubu. Analia vizuri hapa, limetumika neno “Imempasa, yaani , lazima” (1 WAKORINTHO 11:4, 7, 10, 13-14). Hili si taratibu za desturi au mila za Wakorintho kama wengine wanavyojitetea. Tendo hili ni kwa ajili ya malaika. Mbona wanaume wenyewe hatuwaruhusu kuvaa kofia kanisani? Je, kuna andiko gain lingine tofauti na hili linalomkataza mwanaume kufunika kichwa na wanawake kulazimishwa kuwa na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya malaika (kufunika kichwa)?
(xiv) Vibweta vya malashi (ISAYA 3:16-24). Hapa yanazungumziwa mafuta yanayokuwa na harufu kali sana ya kwenda mbali. M,afuta yenye harufu kali sana hayatakiwi. Kujipaka mafuta siyo dhambi (MATHAYO 6:17-18). Lengo la kupaka mafuta ni kuifanya sura au ngozi isipauke(WALAWI 17:15-18). Mtu anaweza kuuliza, mbona Yesu alimwagiwa marhamu (malashi) na akafurahishwa na kitendo hicho? Ni muhimu kufahamu kuwa tendo lile lilikuwa na maana kubwa sana. Yule mwanamke alikuwa anatabiri kifo chake Bwana Yesu. Alikuwa anamuandaa kwa mazishi (MATHAYO 26:7-12). Pia desturi ya wayahudi iliwataka kupaka malashi mtu kabla hajazikwa (YOHANA 19:38-40; MARKO 16:1, 2NYAKATI 16:13-14, MWANZO 49:33,; MWANZO 50:1-3,26). Kwa hiyo, kwa msingi huu wa Neno la Mungu pafyumu zote hazitakiwi. Ni muhimu kufahamu kuwa majini nao wanapenda harufu kali sana
MSINGI WA SABA
KUVAA ILI KUONYESHA DALILI YA KUMILIKI NA KUMILIKIWA
Hakuna ufalme unaotenda kazi bila kuzingatia itifaki. Hata na serikali za duniani tulizonazo leo, mfano serikali yetu ya Tanzania. Katika serikali huwa kuna mtu anayeitwa mkuu wa itifaki, mkuu wa protokali. Kazi yake ni kuhakikisha itifaki inazingatiwa ili mamlaka iweze kutenda kazi. Ni utaratibu ambao unatakiwa kuzingatiwa ili mamlaka iweze kutenda kazi. Huu ni utaratibu wa mamlaka ambao haukuanza leo, hata ufalme wa mbinguni unataka kuona kwamba itifaki inazingatiwa. Ndiyo maana tunapokuwepo kanisani, itifaki lazima izingatiwe kwa ajili ya malaika. Malaika wanataka kuona itifaki ikizingatiwa ili mamlaka ya Mungu ipate kutenda kazi. Kristo awe na sehemu yake, mume kama kichwa awe na sehemu yake na mwanamke awe na nafasi yake (1 WAKORINTHO 14:33). Katika biblia ya tafsiri ya New International Vision 1CORINTHIANS 14:33 NIV). Tunaona kuwa Mungu ni wa utaratibu “Fog God is not a Gog of disorder, but of peace, God is God of order”. Kinachozungumziwa hapa ni namna ya protokali, Mungu anataka mambo yaende kwa order, kwa utaratibu, kwa protokali.
Mungu ameweka protokali yake (1WAKORINTHO 11:3-7, 10, 12-13). Mungu anasema, tukizingatia protokali ya namna hii tutaona jinsi malaika watakavyo tuhudumia. Malaika walifanya kazi za ajabu nyakati za kanisa la kwanza. Waliweza kuwatoa mitume gerezani. Malaika walichangia kwa namna ya ajabu sana katika kuifanya kazi iweze kuwa rahisi. Hata sasa Mungu anasema kuwa malaika ni wahudumu wetu sisi tutakaourithi wokovu (WAEBRANIA 1:13-14). Mal
aika hawatendi kazi nyakati hizi za mwisho kwasababu hatut
aki kuzingatia order (utaratibu). Hatutaki kuzingatia protokali ya Mungu.
Katika utaratibu wa Mungu mwenyewe, mwanaume hatakiwi kufunika kichwa akiwa kanisani au anakuwa katika kuomba na kuhutubu. Na ni kwa ajili ya Kristo. Wanaume wameruhusiwa kuvaa kofia na siyo dhambi kuvaa kofia lakini wanawake biblia haijawaruhusu kuvaa kofia. Wanawake wanavaa vilemba kichwani (vitambaa). Kofia inatajwa katika biblia kuvaliwa na wanaume (KUTOKA 28:1-4, 40; KUTOKA 29:9; KUTOKA 39:27-28; MAMBO YA WALAWI 16:4). Sasa, mwanaume anapokuwa amevaa kofia anapaswa kuivua anapoingia kwenye ibada. Hili linajulikana vizuri. Watu hawajui kuwa andiko hilo linalomtaka mwanaume avue kofia ndilo hilohilo linalomtaka mwanamke kufunika kichwa (1WAKORINTHO 11:5-7, 10, 12-13). Mwanamke anapaswa kuwa na dalili ya kumilikiwa kichwani kwa ajili ya malaika. Siyo kwa ajili ya mila na desturi za wakorintho kama wengine wanavyosema. Ni kwa ajili ya malaika ili wapate kutuhudumia. Malaika wanazingatia sana protokali. Haipendezi mwanamke kumwomba Mungu asipofunika kichwa. Ikiwa hataki kufunika kichwa na anyolewe.
Hatuna budi kukumbuka kwamba, wamisionari wa kwanza kabisa walioleta ukristo katika nchi yetu kwa mfano. Walifundisha kwa uzito sana jinsi ambavyo mwanamke anapokuwa katika ibada, katika maombi, katika kuhubiri, anatakiwa kuwa amefunika kichwa chake kwa kilemba. Na jambo hili lilikuwa la kawaida miaka ya zamani, ndiyo maana hata leo unaweza kuona katika baadhi ya sehemu katika nchi yetu ya Tanzania kwa mfano bado wanazingatia hili. Utaona sehemu za kaskazini mfano Kilimanjaro na sehemu za kusini mfano Mbeya bado kunai ile hali au utaratibu wa kufunika vichwa vyao. Hasa sehemu za vijijini. Na hata wanaenda mbali kwa kufunika vichwa vyao wakiwa nje ya kanisa. Haya yalitokana na mafundisho ya wamisionari wa waliotilia mkazo suala hili la kuzingatia protokali ya Mungu. Wazee wa zamani wanakumbuka hili.
MSINGI WA NANE
MASHINDANO YA MAUMBILE NI MWIKO
WAFILIPI 2:3,14
“Tusifanye jambo lolote kwa mashindano”. Kimsingi andiko hili linazungumzia mashindano ya maumbile. (ZABURI 102:18)” Watu watakaoumbwa watamsifu Bwana”. Siyo kujisifu mwenyewe eti mimi ni mzuri kuliko wengine , tunayemsifu ni Mungu ailiyetuumba. (1WAKORINTHO 4:7) Hatutakiwi kujisifu kwa sababu ni neema ya Mungu kuwa hivyo. Leo hii mashindano ya umis (ya maumbile) yameshaingizwa kanisani kwa visingizio vya Esta. (ESTA SURA YA 1 & 2 ZOTE) Tunaweza kupata picha ya mashindano yaliyofanyika.. Mfalme wa Ahasuero alikuwa mwovu nay eye ndiye aliyeandaa mashindano hayo ili aweze kujipatia mke baada ya mkewe kumgomea kupita mbele za watu ili kujionesha. Walipotafutwa wanawake mabikira ndipo na Esta akajitokeza. Jambo hili haliwezi kutufanya kuhalarisha mashindano ya maumbile katika kanisa.
MSINGI WA TISA
MAMBO YOTE YANAYOFANANA NA HAYO
(WAGALATIA 5:19-21)
MASSAGE
Ukiangalia katika mtandao huu: WWW.wikipedia.org/wiki/Massage
Unaweza kuona jinsi massage inavyoelezewa vizuri.Inaeleza jinsi mtu anavyotomaswatomaswa katika viungo mbalimbali kwa mikono, kwa vidole. Utaona wanawake wanatomaswa na wanaume na wanaume wakitomaswa na wanawake. Hili ni adui ameliingiza kwa visingizio vya kujichua ili watu waingie kwenye uchafu na miili yetu kuifanya kuwa maskani ya mashetani. Lengo la massage ni kutaka kuamsha hisia za mapenzi na kuwafanya watu kuingizwa katika uzinzi na uasherati. Nyakati hizi za mwisho ni nyakati za hatari sana, tunapaswa kuwa makini sana kwa kila kitu kinachoibuka na kukipima kibiblia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni