SOMO: HAMNA KITU KWAKUWA HAMUOMBI
Kabla
yakuendelea kujifunzi somo letu ni vizuri tukafahamu maana halisi ya
maombi,kama tutakavyolitumia sana neno hili ktika somo letu la leo.
Maombi ni
mawasiliano baina ya pande mbili ,baina ya mwenye kuhitaji na mwenye kutoa
msaada au mahitaji mfano mtu unapokwenda kumba mahali pa kulima au
shamba,unapomwendea huyo mwenye mashamba ,wewe unakwenda kama mhitaji na mwenye
shamba kama mtoa msaada.wewe mwenye mahitaji inakubidi ueleze shida yako kwa
rugha yako atayoielewa yule tajili mwenye shamba ili upate kupewa hilo hitaji
lako la shamba.ingawaje kuna kubembeleza au kumshawishi,ili tu hitaji lako
lipatikane.sasa unapofanya hivyo tunasema una fanya maombi.ingawaje huyo mtu
unamwona kwa macho ,tofauti na Mungu yeye hatumwoni kwa macho kama mwanadamu
lakini maombi yetu ni kama tunavyowaomba wanadamu wenzetu kwa kutumia rugha
zetu tulizozizoea.
Na kwa Mungu
nako kuna haja au shida zetu au mahitaji yetu mbalimbali,ambayo ni haki yetu
Mungu kutufanyia.iwe ni katika mwili au katika roho.ni haki yetu kusamehewa
dhambi sisi wanadamu mana tuko katika dunia iliyijaa dhambi na shetani
anatuwinda usiku na mchana.yeremia33:8 Nami
nitawasafisha na uovu wao wote, ambao kwa huo wamenitenda dhambi; nami
nitawasamehe maovu yao yote, ambayo kwayo wamenitenda dhambi, na kukosa juu
yangu. Nihaki yetu kuponywa
magojwa hata kama ni mazito,au tumeyapata kutokana na dhambi zetu.baada yakuokoka
ni haki yetu kuponywa magojwa yote. yeremia
33: 6 Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia
wingi wa amani na kweli. Na
tena katika biblia katka zaburi 103:3 anasema Mungu wetu akusamehe dhambi zako
zote na kukuponya magonjwa yako yote. Nihaki yatu sisi tuliokoka kuoa au
kuolewa,maadamu una sifa za kuoa na kuolewa MUNGU tangia ulipookoka amekupangia
mume wakukuoa au mke wakuolewa na wewe
kama.mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia
msaidizi wa kufanana naye. Ni
haki yetu kubarikiwa katika pesa na kufanikiwa katika biashara na kazi
zetu,familia zetu ,masomo yetu na mambo yetu mbali mbali,kadili tunapozidi
kudumu katika imani hii ya wokovu.soma katika
kumbukumbu la torati 28:3-13. Ndo maana tunaitwa
waliobarikiwa na Mungu,maana tuko katika fungu lake.soma katika. mathayo
25:34 Kisha Mfalme atawaambia
wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni,
mliobarikiwa na Baba yangu, urithini
ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; Sasa hizi baraka za Mungu haziji hivi hivi hata kama tuna haki
kuzipata,na Mungu anajua kuwa ni haki yetu kuzipata hizi Baraka,hasa sisi
tuliokoka.lakini ili kuzipokea na kuziona katika maisha yetu ni lazima tufuate
kanuni yake aliyoweka,kanuni yake
aliyoweka ni maombi,anataka tuombe.anataka tumweleze haja ya mioyo yetu ili
tupate haki zetu.maana ni haki zetu kwetu sisi watoto wa Mungu,lakini anataka
tumweleze ili tupewe.isaya 43:26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa
haki yako.Bila kuomba MUNGU
ANAONEKANA HANA UWEZO KWAKO. Bila kuomba mtoto wa Mungu ni vigumu kumwona
Mungu akihusika na mahitaji yako,hata kama mahitaji yako yanakuumiza sana. Ndo
maana anataka tuombe,hakuna njia nyingine.hakuna watu aliowaweka ili wao waombe
sisi tukae kupokea tu; hakuna! Ndo maana
biblia inasema kila aombaye hupokea,ombeni nanyi mtapewa.Luka 1:9-10 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi
mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila
aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.Mungu
anataka kukusikia wewe unatamka nini mbele zake, katika mahitaji yako na kazi
ya Mungu kwa ujumla.pale unapo nyamaza kimya hutaki kuomba unaonyesha kuwa
huhitaji lolote kutoka kwa Mungu,ina maana unafanana na Mungu wewe, ,yaani
umejitosheleza huna haja na kitu. ni kweli; huna hitaji lolote unalohitaji
kutoka kwa Mungu,ni kweli huna…..HITAJI LOLOTE
..!.. kweli. yapo mengi yaliyotushinda
ebu tuombe!; omba;! Omba omba katika zamu yako.OMBA.bila kuomba hatuwezi kupata
kitu chochote kutoka kwa Mungu wetu. yakobo
4:2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata.
Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Mtu wa Mungu kuna baraka tele kama utakuwa mtu wa
maombi,Bwana akusaidie katika jina la Yesu.
Tusiombe
kama watu wa dini waombavyo kwa kutumia lozari,maji ya baraka au mafuta ya
upako au kupitiA wafu au mbele ya lisanamu,ambalo wanaliita lisanamu la yesu
sijui.namna hiyo hatuwezi ona nguvu ya Mungu yakuijbu maombi yetu.yeye anataka
tuombe kwa namna ilea aliyoiweka yeye yaani jina la Yesu pekee basi. yohana 16:24 Hata sasa hamkuomba neno kwa
jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.Hata kama
unaombewa ,zingatia kuomba wewe kwanza kabla yakuombewa.ndipo utaona nguvu
zaidi za Mungu wa mbinguni.ukiombewa bila kuomba wewe kwanza,unapunguza nguvu
ya Mungu katika maombi yako.hivyo kabla yakuombewa hakikisha umeomba wewe
kwanza.
Ukitaka
kuomba mda mlefu; anza na shukrani kwa
mungu, mwambie mungu akusamehe
nakukutakasa, alafu mwombe roho
mtakatifu akusaidie kuomba, alafu anza
kuomba mbele za Mungu mahitaji yako yote,USISAHAU KUNIOMBEA MCHUNGAJI WAKO. roho akikusaidia kuomba utaona maombi
yanakuwa mepesi sana.Ukimaliza maombi
yako usisahau kushindana na kuhalibu kazi za giza kinyume na maombi yako.
Simama mwambie Mungu akupe neema yake ya kuomba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni