Jumatatu, 13 Juni 2016

HAMNA KITU KWA KUWA HAMUOMBI



SOMO: HAMNA KITU KWAKUWA HAMUOMBI

Kabla yakuendelea kujifunzi somo letu ni vizuri tukafahamu maana halisi ya maombi,kama tutakavyolitumia sana neno hili ktika somo letu la leo.
Maombi ni mawasiliano baina ya pande mbili ,baina ya mwenye kuhitaji na mwenye kutoa msaada au mahitaji mfano mtu unapokwenda kumba mahali pa kulima au shamba,unapomwendea huyo mwenye mashamba ,wewe unakwenda kama mhitaji na mwenye shamba kama mtoa msaada.wewe mwenye mahitaji inakubidi ueleze shida yako kwa rugha yako atayoielewa yule tajili mwenye shamba ili upate kupewa hilo hitaji lako la shamba.ingawaje kuna kubembeleza au kumshawishi,ili tu hitaji lako lipatikane.sasa unapofanya hivyo tunasema una fanya maombi.ingawaje huyo mtu unamwona kwa macho ,tofauti na Mungu yeye hatumwoni kwa macho kama mwanadamu lakini maombi yetu ni kama tunavyowaomba wanadamu wenzetu kwa kutumia rugha zetu tulizozizoea.
Na kwa Mungu nako kuna haja au shida zetu au mahitaji yetu mbalimbali,ambayo ni haki yetu Mungu kutufanyia.iwe ni katika mwili au katika roho.ni haki yetu kusamehewa dhambi sisi wanadamu mana tuko katika dunia iliyijaa dhambi na shetani anatuwinda usiku na mchana.yeremia33:8          Nami nitawasafisha na uovu wao wote, ambao kwa huo wamenitenda dhambi; nami nitawasamehe maovu yao yote, ambayo kwayo wamenitenda dhambi, na kukosa juu yangu.                        Nihaki yetu kuponywa magojwa hata kama ni mazito,au tumeyapata kutokana na dhambi zetu.baada yakuokoka ni haki yetu kuponywa magojwa yote.  yeremia 33: 6 Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.         Na tena katika biblia katka zaburi 103:3 anasema Mungu wetu akusamehe dhambi zako zote na kukuponya magonjwa yako yote. Nihaki yatu sisi tuliokoka kuoa au kuolewa,maadamu una sifa za kuoa na kuolewa MUNGU tangia ulipookoka amekupangia mume wakukuoa au   mke wakuolewa na wewe kama.mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.               Ni haki yetu kubarikiwa katika pesa na kufanikiwa katika biashara na kazi zetu,familia zetu ,masomo yetu na mambo yetu mbali mbali,kadili tunapozidi kudumu katika imani hii ya wokovu.soma katika  kumbukumbu la torati 28:3-13.                  Ndo maana tunaitwa waliobarikiwa na Mungu,maana tuko katika fungu lake.soma katika. mathayo 25:34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;             Sasa hizi baraka za Mungu  haziji hivi hivi hata kama tuna haki kuzipata,na Mungu anajua kuwa ni haki yetu kuzipata hizi Baraka,hasa sisi tuliokoka.lakini ili kuzipokea na kuziona katika maisha yetu ni lazima tufuate kanuni yake aliyoweka,kanuni yake aliyoweka ni maombi,anataka tuombe.anataka tumweleze haja ya mioyo yetu ili tupate haki zetu.maana ni haki zetu kwetu sisi watoto wa Mungu,lakini anataka tumweleze ili tupewe.isaya 43:26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.Bila kuomba MUNGU ANAONEKANA HANA UWEZO KWAKO. Bila kuomba mtoto wa Mungu ni vigumu kumwona Mungu akihusika na mahitaji yako,hata kama mahitaji yako yanakuumiza sana. Ndo maana anataka tuombe,hakuna njia nyingine.hakuna watu aliowaweka ili wao waombe sisi tukae kupokea tu; hakuna!  Ndo maana biblia inasema kila aombaye hupokea,ombeni nanyi mtapewa.Luka 1:9-10            Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.Mungu anataka kukusikia wewe unatamka nini mbele zake, katika mahitaji yako na kazi ya Mungu kwa ujumla.pale unapo nyamaza kimya hutaki kuomba unaonyesha kuwa huhitaji lolote kutoka kwa Mungu,ina maana unafanana na Mungu wewe, ,yaani umejitosheleza huna haja na kitu. ni kweli; huna hitaji lolote unalohitaji kutoka kwa Mungu,ni kweli huna…..HITAJI LOLOTE  ..!.. kweli.  yapo mengi yaliyotushinda ebu tuombe!; omba;! Omba omba katika zamu yako.OMBA.bila kuomba hatuwezi kupata kitu chochote kutoka kwa Mungu wetu.  yakobo 4:2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Mtu  wa Mungu kuna baraka tele kama utakuwa mtu wa maombi,Bwana akusaidie katika jina la Yesu.
Tusiombe kama watu wa dini waombavyo kwa kutumia lozari,maji ya baraka au mafuta ya upako au kupitiA wafu au mbele ya lisanamu,ambalo wanaliita lisanamu la yesu sijui.namna hiyo hatuwezi ona nguvu ya Mungu yakuijbu maombi yetu.yeye anataka tuombe kwa namna ilea aliyoiweka yeye yaani jina la Yesu pekee basi.  yohana 16:24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.Hata kama unaombewa ,zingatia kuomba wewe kwanza kabla yakuombewa.ndipo utaona nguvu zaidi za Mungu wa mbinguni.ukiombewa bila kuomba wewe kwanza,unapunguza nguvu ya Mungu katika maombi yako.hivyo kabla yakuombewa hakikisha umeomba wewe kwanza.
Ukitaka kuomba mda mlefu;  anza na shukrani kwa mungu,    mwambie mungu akusamehe nakukutakasa,     alafu mwombe roho mtakatifu akusaidie kuomba,    alafu anza kuomba mbele za Mungu mahitaji yako yote,USISAHAU KUNIOMBEA MCHUNGAJI WAKO.  roho akikusaidia kuomba utaona maombi yanakuwa mepesi  sana.Ukimaliza maombi yako usisahau kushindana na kuhalibu kazi za giza kinyume na maombi yako.
                  Simama mwambie Mungu akupe neema yake ya kuomba.