Jumamosi, 25 Novemba 2023

SOMO:MKRISTO KAMA SHAHIDI WA MUNGU (ISAY 43:12)

 NENO HILI LIMENIBARIKI SANA.

EBU TUBARIKIWE PAMOJA.

SOMO:MKRISTO KAMA SHAHIDI WA MUNGU

(ISAY 43:12)

Kila siku Mungu anatoa tangazo la kuokoa pale alipo mkristo ili watu waione kazi yake.

Kila tangazo linapotoka tu,shetani lazima aweke pingamizi kama alivyofanya kwenye tangazo la Ayubu(Ayub 1:8-11).

Tangazo hili ni la kisheria kama mahakamani hivyo lazima iamuliwe na sheria ya Mungu(Isay 43:9).

Lazima Mungu alete shahidi ili kuthibitisha tangazo lake.

Eneo la mahakama ni pale tulipo kazini,shuleni,nyumbani.

Mungu anapomleta shahidi mwaminifu kupitia maisha ya shahidi anapata ushindi na kuongeza waenda mbinguni(Isay 8:2).

Shahidi wake anapothibitsha maneno ya Shetani kwsmba ni ya kweli kupitia maisha yake basi shetani anaongeza waenda motoni.

Kazi ya shetani ni kutembea kila mahali alipo mkristo kukusanya ushahidi ili kushinda kesi zake

Ndio maana lijua maishaya Ayubu kwamba amelindwa kwa uzio maana alishawai kifika na kukuta uzio(Ayb 1:10).

Anachunguza simu zetu zote nini tunaangalia kwenye mtandao,msg zetu zote,namba za simu tulizonazo,maongezi yetu yote.

Kazi hii 

hufanywa kisheria kama wafanyavyo POLICE(Peoples organization of law investigation in criminal evidence).

Sheria hapa ni neno la Mungu maana hukumu ya mwisho itaamuliwa na ushahidi usio na chembe ya shaka kama ilivyotokea kwa Ayubu.

Ayubu bila kujua kilichokuwa kikiendelea upande wa Mungu na shetani alijikuta akithitisha kwamba Mungu anaokoa na shetani ni mwongo.

Kuna kesi zinaendelea kila siku dhidi yetu upande wa pili bila sisi kujua.

Hakuna kitu kinaochoima pale unapomleta shahidi wahakamani kisha anakukandamiza.wewe.

Mungu wetu anajivunia mashahidi waaminifu kama Ayubu kama watu wanavyojivunia ndugu zao wenye uwezo wa kifedha.

Wengine wanatambia ndugu zao wanaofanya kazi idara fulani ktk serikali.

Mungu pia anatutambia sisi kama alivyomtangaza Ayubu mbele za shetani.

Tujiulize je shetani akija kuchunguza mali zetu na pesa zetu atapata ushahidi au ataambulia patupu kwamba sisi hatuibi zaka na sadaka?

Hiyo ndio humpa Mungu ushindi wa kishindo kwamba anao akina Ayubu wa leo.

Hivyo kuanzia leo tuongee kama shahidi maana maneno yetu yatapelekwa mahakamani.

Tutumie simu zetu kama mashahidi tukijua polisi wa kiroho anakusanya ushahidi kila siku.

Mafundisho ya mavazi yanatumiwa kila siku kukusanya  ushahidi ili Mungu athibitishe kwamba hana makahaba(Mith 7:10).

Shahidi ndiye tegemeo la kushinda kesi.

Ndoa zetu nikituo cha mahakama kila siku na adui yetu ameshakusanya vurugu zetu zote.

Nafasi tuliyonayo ni kutubu kwa kumaanisha na kuanza upya.

Toba ni kufuta ushahidi ili akifika mahakamani akute faili tupu na kesi itupiliwe mbali.

Tutubu sasa ili atusamehe sasa na kutuokoa sasa(2kor 6:1-2).