MSAMAHA UPO!
Watu wengi huwa wanamwona Mungu kama wanavyowaona wanadamu,wamefika mbali zaidi na kuwaza kuwa hata katika msamaha nako ni hivyo hivyo.Biblia inasema Mungu sio kama wanadamu, Hesabu 23:19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Katika msamaha anasemaje katika neno lake.Danieli 9:9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; msamaha wake ni tofauti na misamaha yoyote kutoka popote na kwa yeyote,Yeye anaposamehe anasamehe na kusahau kabisa.Isaya 43:25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. Kumbuka wanadamu wao wakisamehe hawasahau. lakini Mungu ni tofauti kabisa anasamehe na kusahau kabisa ,akikusamehe unakuwa kama hujawai kutenda dhambi.
Lakini ili mtu asamehewe lazima atubu akiwa amemanisha kuacha dhambi toka moyoni.hata kama ni dhambi nyingi kiasi gani utasamehewa zote.Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.tubu hivi :MUNGU BABA MIMI MWENYE DHAMBI, NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE,NATUBU KWAKUMANISHA KUZIACHA.NIPE NA UWEZO WAKUSHINDA DHAMBI,KATKA JINA LA YESU ASANTE KWAKUNISAMEHE, AMENI.