Jumatatu, 10 Agosti 2015

SHUHUDA ZA MATENDO MAKUU YA YESU.


YESU AMETENDA MENGI SANA KATKA MAISHA YA WATU MBALIMBALI HAPA DUNIANI,MDA SI MLEFU UTAPATA SHUHUDA MBALIMBALI.
za uponyaji, za wengi waliokolewa na Yesu,za mikutano mbali mbali inayofanyika huko vijijini hasa mkoa wa mara,Hata wale ambao Bwana Yesu amebadilisha maisha yao toka dhambini  na sasa wameokoka.
Elioth ngumba,akiwa na Baba yake mzazi,mzee ashery ngumba.

Ijumaa, 3 Julai 2015

BAADA YA KUFA ;NI HUKUMU.



BAADA YA KUFA ;NI HUKUMU.
Namshukuru Mungu wa Bwana wetu Yesu kristo,aliyetufanya kuwepo siku kama ya leo.Namshukuru tena kwa neema kubwa aliyotupa kutafakari juu ya uwepo wake,neema hii ndio iliyotufanya leo uone ukurasa huu na kuzisoma habari hizi njema sana.Hasa kutakari juu ya kule ambako kila mwanadamu antalajia kuwa siku moja nae atakufa ataondoka duniani.Na Mungu wa mbinguni anapenda sa na kila mtu ajue kwamba ipo siku ataondoka duniani,ili ajiweke tayari.2 koritho 4:18 tusiviangalie vinavyoonekana,bali visivyoonekana .kwa maana vinavyoonekana ni vya mda tu ;bali visivyoonekana ni vya milele.
NINI MAANA KUFA:-
Maana rahisi ya kufa ni mwili kutenganishwa na uhai,kwa namna rahisi; katika miili yetu kuna uhai unaotufanya tuwe hai.miili yetu ni udongo ni mavumbi,Mungu alipokuwa anamfanya mwanadamu alitumia mavumbi ya nchi yaani udongo.Alafu akapuliza ndani ya huo udongo aliouumba pumzi ya uhai ,mtu akawa nafsi hai. Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu akawa nafsi hai
Mtu anapokufa sasa ule uhai unamrudia yeye aliyeutoa,yaani Bwana Mungu.mhubiri 12:7 Nayo mavumbi kuiridia nchi kama yalivyokuwa,Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Ule uhai, ni nafsi ya mtu inayojitambua kwamba yeye ni nani. Maana inakuwa katika mwili wa roho. Iko miili ambayo mtu anapokufa anavikwa, inaitwa miili ya roho.1 koritho 15:44………………ikiwa uko mwili wa asili na waroho pia uko
Inavyokuwa mtu anapokufa ni kwamba,anahamishwa kutoka katika mwili huu wa asili ,tunaozaliwa nao;alafu roho au uhai wake ,unamiminwa kwenye mwili wa roho usiokufa tena.2 Timotheo2:6 Kwamaana,mimi sasa namiminwa,na wakati wakufariki kwangu umefika.Kinacholala kabrini ni mwili huu wa asili,ambao ni udongo,lakini uhai wa yule mtu,haubaki kaburini.Unamiminwa katika mwili mwingine wa roho,bila kujali huyo mtu alikuwa anamjua Mungu au alikuwa hamjui.Angalia kisa cha masikini lazalo natajiri,japo kuwa wote walikufa,lakini wote waliendelea kuishi katika ulimwengu wa roho. [luka 16:22-25,] Ndo maana Biblia katka, Ayubu 19:26…………pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Bwana.
Nadhani mpaka hapa mpendwa umeshaelewa kwa ufu maana ya kufa.
BAADA KUFA HUKUMU:-
Waebrania 9:27N kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja,na baada ya kufa hukumu.
Tumezoea maneno kama haya,mlaze mahala pema peponi,bila kujari huyo mtu alikuwaje.Hata pale mhubiri kwenye msiba anapojisahau kutamka maneno hayo ya mweke mahali pema peponi,wafiwa hajisikii vizuri,wanaona kama ndugu yao amezuiliwa kwenda peponi.Kumbuka mpendwa mwanadamu hana ruhusa yakuwapeleka watu peponi,zaidi anawaelekeza njia ya kwenda peponi,kama ninavyofanya mimi katka haya uyasomayo sasa hivi.ebu tuendelee;
Mtu anapokufa tu mda huo huo anapewa malipo ya kazi zake kwamba ni mbovu au ni njema,Biblia inasema katika Warumi 6:23 mshara wa dhambi ni mauti;bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.mtu baada ya kufa tu anapewa mshahara wake ambao ni mauti.Hii mauti sio kifo,nikutupwa katika moto wa milele,kwenye mateso yasiyoelezeka,angalia [Ufunuo 21:8] hapa sasa hakuna cha usomi,utjiri,umalufu nk,ukifa katika dhambi ni jehanum ya moto.Ndo maana Mungu anatushaangaa tunapohangaikia umarufu wa dunia hii,wakati tunajua ipo siku tutakufa.Mwenye akili anatafuta maisha mazuri ya baada ya kufa maana hayo ni ya milele.fanya hivi dhambi zinaondoka kwa mtu pale anapotubu na kuziacha,anaeondoa dhambi ni Yesu mwenyewe,tubu leo utasamehewa bure kabisa !!

pastor ELIOTH NGUMBA

Ongeza kichwa

Alhamisi, 7 Mei 2015

MSAMAHA UPO!
Watu wengi huwa wanamwona Mungu kama wanavyowaona wanadamu,wamefika mbali zaidi na kuwaza kuwa hata katika msamaha nako ni hivyo hivyo.Biblia inasema Mungu sio kama wanadamu, Hesabu 23:19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Katika msamaha anasemaje katika neno lake.Danieli 9:9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; msamaha wake ni tofauti na misamaha yoyote kutoka popote na kwa yeyote,Yeye anaposamehe anasamehe na kusahau kabisa.Isaya 43:25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. Kumbuka wanadamu wao wakisamehe hawasahau. lakini Mungu ni tofauti kabisa anasamehe na kusahau kabisa ,akikusamehe unakuwa kama hujawai kutenda dhambi.
Lakini ili mtu asamehewe lazima atubu akiwa amemanisha kuacha dhambi toka moyoni.hata kama ni dhambi nyingi kiasi gani utasamehewa zote.Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.tubu hivi :MUNGU BABA MIMI MWENYE DHAMBI, NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE,NATUBU KWAKUMANISHA KUZIACHA.NIPE NA UWEZO WAKUSHINDA DHAMBI,KATKA JINA LA YESU ASANTE KWAKUNISAMEHE, AMENI.